Storm FM

Wafanyabiashara Geita walalamikia utitiri wa kodi

13 August 2024, 4:35 pm

Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) CPA  Yusuph Mwenda akizungumza na wafanyabiashara katika ukumbi wa Otonde. Picha na Edga Rwenduru

Wafanyabiashara wa madini mkoani Geita wameiomba serikali kupunguza utitiri wa kodi katika biashara ya madini kwani imekuwa chanzo cha baadhi ya wafanyabiashara kutorosha madini kwa lengo la kukwepa kodi.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Baadhi ya wafanyabiashara wa madini mkoani Geita Agosti 12, 2024 wamefanya mkutano na kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) CPA  Yusuph Mwenda ambaye yupo mkoani Geita kwaajili ya ziara ya kusikiliza kero mbalimbali za wafanyabiashara.

Wameeleza changamoto kubwa imekuwa ni mlundikano wa kodi ambazo zinawanima uhuru wa kufanya biashara na kuiomba mamlaka kuangalia suala hilo

Sauti ya wafanyabiashara
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Otonde mjini Geita. Picha a Edga Rwenduru

Katika hatua nyingine wameiomba serikali kuwawajibisha baadhi ya watumishi wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Geita wanaotumia lugha zisizofaa sambamba na kutoa maneno ya vitisho kwa wafanyabiashara.

Sauti ya wafanyabiashara

Kamishna mkuu  wa TRA Yusuph Mwenda amesema kipaumbele cha kwanza cha TRA ni kurahisisha ufanyikaji wa biashara na kubadilisha mifumo ya kodi inayolalamikiwa.

Sauti ya kamishna mkuu TRA