Storm FM

Taasisi za fedha zakumbushwa kuwainua wakulima

13 August 2024, 9:59 am

Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt. Dotto Biteko akizungumza katika hafla uzinduzi wa KCB Bank Geita. Picha na Kale Chongela

Serikali yahimiza taasisi za kifedha nchini kutokuwabagua wakulima kwani kwa kuwawezesha itasaidia kukuza sekta ya kilimo nchini kwa ujumla.

Na: Kale Chongela – Geita

Taasisi za kifedha zimetakiwa kuwapa kipaumbele wakulima katika suala la mikopo ili kukuza uchumi wa kila mmoja na taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt. Doto Biteko Agosti 12, 2024 akiwa katika hafla ya uzinduzi wa KCB bank iliyopo Mjini Geita ambapo ameeleza kuwa ili Tanzania iendelee kukua kiuchumi ipo haja ya taasisi hizo kutoa fursa kwa wakulima.

Sauti ya waziri Biteko
Viongozi mbalimbali wa mkoa wakiongozwa na naibu waziri mkuu Biteko wakishiriki katika zoezi la kukata utepe kuashiria uzinduzi wa KCB Bank. Picha na Kale Chongela

Mkurugenzi wa biashara wa kanda KCB group na mkurugenzi mtendaji wa KCB benki nchini Tanzania Bw. Cosmas Kimario amesema KCB benki imeanzishwa mwaka 1997 kwa Nchi ya Tanzania na ina matawi 17 na kwamba ina lengo ni kuendelea kupanua wigo mpana wa biashara za kibenki.

Sauti ya mkurugenzi

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi Mkoani Geita kujenga desturi ya kutunza fedha zao sehemu salama ikiwemo benki.

Sauti ya RC Geita