Storm FM

Vumbi lawa kikwazo kwa watumiaji wa stendi Geita mjini

9 August 2024, 9:48 am

Muonekano wa eneo la stendi ya mjini Geita ambayo inatumiwa na wananchi. Picha na Kale Chongela

Miundombinu mibovu kwenye stendi ya magari ya abiria mkoani Geita imetajwa kuwa kikwazo kwenye utoaji wa huduma.

Na: Kale Chongela – Geita

Watumiaji wa kituo kikubwa cha magari ya abiria mkoani Geita wamedai kukabiliwa na uwepo wa vumbi linalosababishwa na ubovu wa stendi hiyo.

Baadhi ya madereva waliopo katika eneo hilo wameelekeza kilio chao kwa serikali kuona namna ya kutatua changamoto hiyo ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.

Sauti ya madereva

Sanjari na hayo baadhi ya wajasiriamali ambao wanafanya shughuli ndogo ndogo za kiuchumi katika eneo hilo wameeleza changamoto hiyo inapelekea bidhaa zao kujaa vumbi kwa wakati wote hali inayohatarisha afya za watumiaji.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita Yefred Myenzi akiwa katika mahojiano maalumu katika kipindi cha Storm asubuhi Agosti 08, 2024 amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kufafanua kuwa mikakati waliyonayo ni kujenga stendi kubwa katika eneo la mji wa kiserikali Magogo.

Sauti ya Mkurugenzi