Storm FM

Geita kuanza mikakati ukarabati barabara zilizoharibiwa na mvua

7 August 2024, 1:45 pm

Mkuu wa mkoa wa Geita Martin Shigela akiwa katika zoezi la utiaji saini mikataba na wakandarasi. Picha na Edga Rwenduru

Kufuatia mvua za masika zilizonyesha kwa mwaka 2024 kuacha uharibifu kwa baadhi ya miundombinu ya barabara, serikali mkoa wa Geita yaanza mikakati ya matengenezo.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Serikali kupitia wakala wa barabara mijini na vijijini TARURA mkoa wa Geita imeingia mkataba na wakandarasi 24 kwaajili ya ukarabati na ujenzi wa barabara zilizoharibiwa na mvua kipindi cha Masika.

Akizungumza wakati wa tukio la kusaini mikataba hiyo na wakandarasi hao Augost 5, 2024 katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita, meneja wa TARURA mkoa wa Geita mhandisi David Msechu amesema mkataba huo una thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 9.

Sauti ya meneja TARURA

Mhandisi Ezekiel Festo ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Rumanyika investment akizungumza kwa niaba ya wakandarasi wengine ameiomba serikali kutazama upya kipengele cha faini endapo mkandarasi atachelewesha mradi na kile cha mwajiri kuwajibika endapo atachelewesha malipo kwa mkandarasi.

Sauti ya mkandarasi

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela wamewataka wakandarasi hao kutekeleza na kukamilisha miradi kwa wakati.

Sauti ya RC Geita