Storm FM

Mwitikio wa uchangiaji damu bado mdogo mjini Geita

6 August 2024, 12:13 pm

Hospitali ya halmashauri ya mji wa Geita mkoani Geita. Picha na mwandishi wetu kutoka maktaba

Uhitaji wa damu salama katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Geita bado ni mkubwa ukiliganisha na wahitaji kwani kwa siku hutumika unit 20 hadi 25.

Na: Kale Chongela – Geita

Mratibu wa kitengo cha damu salama katika hospitali hiyo Dkt. Shaban James Makoye Agosti 03, 2024 akiwa katika kongamano la waumini wa kanisa la wasabato maarufu “makambi” ambalo limefanyika katika uwanja wa EPZA Bombambili mjini Geita ametoa wito kwa wananchi kuendelea kujitokeza katika uchangiaji wa damu salama

Sauti ya mratibu

Sambamba na kongamano hilo baadhi ya wananchi na waumini  wamejitoa kuchangia damu huku wakieleza kuwa upo umuhimu kwa kila mmoja kujitoa ili kusaidia wagonjwa wenye uhitaji.

Sauti ya wananchi

Katibu wa kamati ya afya na mazingira katika kambi ya waadventist wasabato Gabriel Peter Wagese amesema jumla ya makanisa 26 kutoka halmashauri ya mji wa Geita yamekusanyika kwa lengo kufundishana neno la Mungu kama ilivyo desturi ya dini hiyo.

Sauti ya katibu afya