Storm FM

Afariki dunia baada ya kujeruhiwa na kiboko

30 July 2024, 5:58 pm

Ndugu na majirani wakiwa katika msiba kuifariji familia. Picha na Edga Rwenduru

Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Nyiri Katelezi (40) mkazi wa kijiji cha Nyandago kata ya Butundwe wilaya ya Geita mkoani Geita amefariki dunia baada ya kujeruhiwa vibaya na mnyama.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Tukio la kujeruhiwa mwanaume hiyo limeokea Julai 27, 2024 majira ya saa 11 alfajiri ambapo alikuwa akiendelea na shughuli yake ya uvuvi kama ilivyo desturi ya kila siku katika mwalo wa Nyandago.

Mbunge wa Busanda Mhandisi Tumaini Magesa akizungumza na msemaji wa familia iliyopata msiba. Picha na Edga Rwenduru

Msemaji wa familia hiyo Martine Mulengosha amesema familia imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mtoto wao huku akiiomba serikali kupitia kitengo cha maliasili kutafuta jinsi ya kudhibiti wanyama hao kwani wanyama hao kwa sasa ni tishio kwa wakazi wa kijiji hicho.

Sauti ya msemaji wa familia

Baadhi ya wavuvi na wananchi waliokuwepo katika eneo la tukio ambao wamenusurika katika tukio hilo wanasimulia namna lilivyojitokeza.

Sauti ya wananchi
Ndugu na majirani wakiwa katika msiba kuifariji familia. Picha na Edga Rwenduru

Mbunge wa jimbo la Busanda mhandisi Tumaini Magesa baada ya kufika nyumbani kwa wafiwa ametoa mkono wa pole huku akisema kuwa tayari mamlaka husika imeanza kufuatilia wanyama hao ili kutatua changamoto hiyo.

Sauti ya mbunge