Storm FM

Mama anyonga mtoto wake hadi kufa Geita

27 July 2024, 12:54 pm

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Kamishna msaidizi mwandamizi (SACP) Safia Jongo.

Kwa mujibu wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita kuanzia kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu 2024 yameripotiwa matukio 32 ya ukatili ambapo watuhumiwa 7 wamehukumiwa.

Na: Mrisho Sadick – Geita

Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Flora Mapolu (33) mkazi wa kitongoji cha Mlima namba tano kata ya Lwamgasa wilayani Geita kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wake mwenye umri wa miezi miwili, tukio lililotokea Julai 22, 2024 katika kitongoji cha Miyenze, kata ya katome wilayani Bukombe mkoani Geita.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema walipata taarifa za uwepo wa mwili wa mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi miwili ambaye aliuawa kwa kunyongwa shingo kisha kukatwa viungo vyake ambavyo ni mkono wa kulia na mguu wa kulia kisha mwili wake kutelekezwa katika njia inayopitia shambani kwenda kisimani.

Sauti ya SACP Safia Jongo

Katika tukio lingine, Rehema Paulo (26) mkazi wa kata ya Katente wilaya ya Bukombe amejeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu za kichwani na kukatwa viganja vya mikono yake huku chanzo cha tukio hilo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Sauti ya SACP Safia Jongo

SACP Jongo amesema Rehema kwasasa anaendelea kupatiwa matibabu hosptali ya wilaya ya Bukombe na Jeshi hilo linaendelea kumsaka baba Lawi kwa tuhuma za kuhusika na tukio hilo na kwamba baba huyo pamoja na mke wake wametoroka baada ya tukio hilo kutokea