Storm FM

Wakazi Nyantorotoro waibuka na jipya baada ya barabara kutengenezwa

23 July 2024, 7:51 am

Barabara iliyofanyiwa marekebisho na TANROADS ili kudhibiti mwendo kasi. Picha na Kale chongela

Mnamo mwezi Mei mwaka huu wakazi wa Nyantorotoro A walifunga barabara kuu ili kushinikiza matengenezo ya barabara hiyo kutokana na kuchoshwa na ajali za mara kwa mara eneo hilo.

Na: Kale Chongela – Geita

Baada ya TANROADS kufanya marekebisho ya barabara hiyo, watumiaji wa vyombo vya moto wanatumia eneo la watembea kwa miguu wakiwa na vyombo vya moto

Wakazi wa mtaa wa Nyantorotoro A wanaoishi pembezoni mwa barabara katika eneo la mwembeni kata ya Nyankumbu mjini Geita wakizungumza na Storm FM Julai 22, 2024 wameiomba TANROADS mkoa wa Geita kuziba upya sehemu ambayo baadhi ya madereva wanapita pembezoni mwa barabara.

Sauti ya wananchi

Mmoja wa madereva wa bajaji ambaye anatumia barabara hiyo ameeleza sababu ambazo zinapelekea baadhi ya madereva kupita pembezoni mwa barabara

Sauti ya dereva

Meneja TANROADS mkoa wa Geita ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano pindi wanapoona madereva wanakiuka hilo

Sauti ya meneja TANROADS