Bodaboda mjini Geita watakiwa kuzingatia sheria
20 July 2024, 10:32 am
Usafiri wa pikipiki maarufu bodaboda umeendelea kurahisisha maisha ya watu ambapo umekuwa ukitumika mara nyingi na kutoa ajira kwa vijana wengi.
Na: Kale Chongela – Geita
Madereva pikipiki mjini Geita wametakiwa kuendelea kuzingatia taratibu ambazo wamekuwa wakipewa kwenye vikao vyao ili kuondokana na changamoto ya wao kuporwa vyombo vyao vya usafiri.
Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa chama cha wasafirishaji mjini Geita Benjamini Philibert Julai 19, 2024 akiwa ofisini kwake ambapo ameiambia Storm FM kuwa pamekuwepo na changamoto ya baadhi ya madereva kuporwa pikipiki zao na kundi la watu wasiojulikana .
Mateso Sheria ni dereva pikipiki amebainisha kuwa changamoto hii imekuwa ikiwaathiri kiuchumi huku akitumia fursa hiyo kuwaomba madereva wezake kuendelea kutoa ushirikiano.