Storm FM

Mwanamke adaiwa kufariki katika egesho la bodaboda mjini Geita

19 July 2024, 4:51 pm

Askari wa jeshi la zimamoto na uokoaji mjini Geita wakipandisha mwili wa mwanamke huyo kwenye gari baada ya kufika eneo la tukio. Picha na Edga Rwenduru

Katika hali ya kushangaza Mwanamke mmoja ambaye hajafahamika jina lake anadaiwa kufariki dunia baada ya kuanguka ghafla katika egesho la waendesha pikipiki.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Tukio hilo limetokea Julai 15, 2024 katika mtaa wa uwanja kata ya Nyankumbu mkoani Geita na kuzua taharuki taharuki kwa wananchi waliokuwa katika eneo hilo.

Wananchi waliokusanyika katika eneo la tukio wakiwemo madereva pikipiki. Picha na Edga Rwenduru

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika tukio hilo wamesema tukio hilo limetokea majira ya mchana ambapo mwanamke huyo alianza kuonekana katika eneo hilo siku moja kabla ya tukio hilo na hawatambui makazi yake ni wapi.

Sauti ya mashuhuda

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa uwanja Enos Chelehani amewaomba wananchi kujenga utamaduni wa kutoa taarifa pindi wanapoona hali isiyo ya kawaida.

Sauti ya mwenyekiti
Msemaji wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita Bahati Lugodisha. Picha na Edga Rwenduru

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Geita kwa kushirikiana na Jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuubeba mwili wa mwanamke huyo na kuupeleka hospitali kwaajili ya uchunguzi.

Sauti ya msemaji jeshi la zimamoto