Storm FM

Kijana (16) adaiwa kuuawa na marafiki zake Geita

18 July 2024, 3:49 pm

Baba wa marehemu Adam Selemani akizungumza na mwandishi wetu Evance Mlyakado. Picha na Edga Rwenduru

Matukio ya ukatili mkoani Geita ikiwemo vitendo vya mauaji vimeendelea kuacha simanzi na maswali kwa jamii pindi matukio hayo yanapotokea.

Na: Edga Rwenduru – Geita

Kijana aliyefahamika wa jina la Lisborn Adam Selemani (16) mkazi wa mtaa wa Nyerere Road Kata ya Kalangalala Halmashauri ya mji Geita mkoani Geita ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na vijana wanaosadikika kuwa ni marafiki zake.

Mazingira ya nyumbani kwa wazazi wa marehemu alipokuwa akiishi. Picha na Edga Rwenduru

Baba mzazi wa kijana huyo Adam Seleman amesema kijana wake alichomwa na kitu kinachosadikika kuwa ni kisu wakati akiwa na  marafiki zake majira ya jioni siku ya jumapili ya Julai 7, 2024 wakiwa maeneo ya machinjio ya zamani mtaa wa Ujamaa.

Baada ya tukio hilo, kijana huyo alipelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita na kufanyiwa upasuaji mara tatu ndipo siku ya Jumapili ya Julai 14, 2024 kijana huyo alipoteza maisha.

Sauti ya baba wa marehemu

Mwajabu Omary ni jirani wa familia na mkazi wa mtaa wa Nyerere Road wanaeleza walivyopokea taarifa hiyo.

Sauti ya jirani
Afisa mtendaji wa mtaa wa Nyerere road George Maguga. Picha na Edga Rwenduru

Afisa Mtendaji wa mtaa wa Nyerere road George Maguga amesema mpaka sasa uongozi wa mtaa huo kwa kushirikiana na polisi kata ya kalangalala waliwakamata vijana watatu kwa tuhuma za tukio hilo.

Jeshi la polisi lilifika nyumbani kwa marehemu na kuzungumza na baba wa familia ikiwa ni sehemu ya kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.