Storm FM

Watano wakamatwa mauaji ya mwenyekiti Mwatulole

17 July 2024, 10:13 am

SACP Safia Jongo akiwa katika mahojiano katika studio za Storm FM. Picha na Kale Chongela

Storm FM inaendelea na kampeni ya kupinga ukatili iitwayo “INATOSHA PINGA UKATILI” yenye lengo la kuikumbusha Jamii kutoendelea kufumbia macho matukio ya ukatili.

Na: Ester Mabula – Geita

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo amesema jeshi la polisi limewakamata watu watano wanaotuhumiwa juu ya mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa mtaa wa Mwatulole Noel Ndasa aliyeuwawa kwa kujeruhiwa kwa kukatwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake akiwa nyumbani kwake mnamo June 23, 2024.

Kamanda Jongo ameeleza hayo akiwa katika kituo cha redio cha Storm FM leo Julai 17, 2024 kupitia kipindi cha Storm Asubuhi alipokuwa akifanyiwa mahojiano maalumu.

Sauti ya RPC Geita

Katika hatua nyingine Kamanda Jongo amewasihi wananchi kuendelea kufichua vitendo vya Ukatili huku akitaja sababu ambazo zimekuwa zikitajwa kuwa chanzo cha matukio hayo ya Ukatili.

Sauti ya RPC Geita

Lengo la Storm FM kuanzisha kampeni ya kupinga ukatili iitwayo “INATOSHA PINGA UKATILI”ni kufuatia vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikijitokeza ikiwemo matukio ya ukatili kwa watu wenye ualbino.