Kata ya Ihanamilo yakabiliwa na uhaba wa maji
13 July 2024, 12:38 pm
Licha ya serikali kufanya jitihada za ujenzi wa matundu ya vyoo katika shule zilizopo kata ya Ihanamilo, eneo hilo linakabiliwa na changamoto ya uhaba wa maji.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Changamoto ya uhaba wa maji katika kata ya Ihanamilo halmashauri ya mji wa Geita inapelekea wanafunzi kushindwa kufanya usafi wa vyoo vya shule kwa wakati na kuwaweka hatarini kupata magojwa ya mlipuko.
Hayo yamebainishwa na afisa elimu kata ya Ihanamilo Simon Shija na diwani wa kata hiyo Joseph Rugahila Julai 11, 2024 wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Geita mjini Costantine Kanyasu alipotembelea katika shule ya msingi ikulwa kukagua ujenzi wa matundu 17 ya vyoo unaoendelea katika eneo hilo.
Changamoto ya maji katika kata hiyo haiathiri taasisi ya elimu pekee bali hata wananchi wa kawaida, Emiliana Katemi na Butimanye Malagilo ni wakazi wa kijiji cha Nyakahengere ambao pia wanaeleza changamoto hiyo inavyoathiri maendeleo ya familia kutokana na kutembea umbali mrefu kutafuta maji
Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Costantine Kanyasu anabainisha mikakati ya kutatua changamoto hiyo.