Storm FM

GGML yaanza maandalizi ya Kili challenge 2024

8 July 2024, 10:07 am

Wafanyakazi wa GGML na washiriki wa kupanda mlima Kilimanjaro kwa mwaka 2024. Picha na Kale Chongela

Kampeni ya Kili challenge huratibiwa na mgodi wa dhahabu wa Geita Gold mine limited (GGML) kwa kushirikiana na tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) ambapo hufanyika Julai ya kila mwaka.

Na: Kale Chongela – Geita

Uongozi wa mgodi wa Geita Gold Mine Limited (GGML) umefanya hamasa kwa wananchi wa wilaya ya Chato mkoani Geita kwa lengo la kushirikiana kupanda mlima Kilimanjaro ifikapo Julai 19 mwaka huu.

Akizunguza na waandishi wa habari  Julai 06, 2024 baada ya usafi wa mazingira sambamba na zoezi la upandaji miti katika hospitali ya wilaya ya Chato, meneja mahusiano wa GGML Bw. Gilbert  Moria amesema kwa mwaka huu wanatarajia kuwa na wapanda mlima 70.

Sauti ya Gilbert Moria
Zoezi la upandaji miti katika hospitali ya wilaya ya Chato. Picha na Kale Chongela

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Chato Dkt. Herieth Majaliwa ametumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa GGML kushiriki kufanya usafi sambamba na kupanda miti katika eneo hilo.

Sauti ya mganga mfawidhi Chato

Kwa upande wake meneja wa afya, usalama na mazingira wa GGML Dkt. Kiva Mvungi amesema fedha ambazo zinapatikana kutokana na zoezi la upandaji mlima kilimanjaro husaidia mapambano dhidi ya UKIMWI hapa nchini na kwamba wanatarajia kukusanya bilioni 2.6.

Sauti ya Kiva Mvungi