Storm FM

Wakulima wa nanasi Sungusira walia ugumu wa soko

3 July 2024, 10:16 am

Nanasi zikiwa katika soko kwa ajili ya taratibu za uuzwaji kijiji cha Sungusira. Picha na Evance Mlyakado

Halmashauri ya wilaya ya Geita katika vijiji vya Nzera, Sungusira na Igate vinatajwa kwa ulimaji wa nanasi ambapo baadhi ya wananchi hujihusisha na kilimo hicho ili kujipatia kipato.

Na: Evance Mlyakado – Geita

Changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika kwa wakulima wa zao la nanasi katika vijiji vya Sungusira na Igate kata ya Nzera wilayani Geita imetajwa kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea kushuka kwa mwamko wa wananchi kujihusisha na ukulima wa zao hilo.

Wakulima hao wamebainisha hayo Julai 2, mwaka huu ambapo wamesema wameendelea kupaza kilio chao kwa viongozi na wawekezaji kuwajengea kiwanda kitakachotumia zao hilo kama malighafi kwa lengo la kuwa na soko la uhakika kwa wakulima wa zao hilo.

Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara ya anasi kijijini hapo na mwenyekiti wa Kitongoji wameeleza hatua kadhaa zilizopo katika kuondoa changamoto hiyo

Sauti ya mwenyekiti umoja
Sauti ya mwenyekiti wa kitongoji

Akizungumza kwa njia ya simu katibu tawala msaidizi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita anayeshugulikia masuala ya viwanda, biashara na uwekezaji Bw. Charles Chacha amesema kuwa serikali ipo katika mchakato wa kuweka kiwanda cha uzalishaji wa mazao yatokanayo na zao hilo.

Sauti ya katibu tawala msaidizi