Makampuni ya ulinzi Geita yatakiwa kuhakikiwa
27 June 2024, 4:14 pm
Jeshi la polisi mkoani Geita limeagiza madiwani wote katika halmashauri zote za mkoa wa Geita kuhakikisha wanahakiki makampuni ya ulinzi yaliyopo katika maeneo yao ili kuepukana na vitendo vya uhalifu.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Geita SACP Safia Jongo alipokuwa akizungumza katika vikao maalumu vya vya baraza la madiwani wa halmashauri zote za mkoa wa Geita vya kujadili taarifa ya mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG kwa mwaka 2022/2023
SACP Safia Jongo amesema kuwa vitendo ili kudhibiti vitendo vya uhalifu  vinavyoweza kujitokeza kutokana na baadhi ya makampuni hayo kuajiri wafanyakazi wasio waaminifu wanaoshiriki katika matukio ya uhalifu.
Aidha Kamanda Jongo ameagiza viongozi wa mtaa kuanzisha madaftari ya kudumu ya wakazi na wageni ili kubaini waarifu katika maeneo yao
Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela ametoa ufafanuzi juu ya tofauti ya daftari la kudumu la wakazi na wageni na daftari la kudumu la wapiga kura.