Sakata la mgomo wafanyabiashara lafika Katoro Geita
27 June 2024, 2:21 pm
Sakata la mgomo kwa wafanyabiasha lililoanzia soko la kariakoo jijini Dar es salaam limeendelea kuchukua sura mpya katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
Na: Evance Mlyakado – Geita
Wafanyabiashara wa Mamlaka ya mji mdogo wa Katoro mkoani Geita jana Juni 26, 2024 wameungana na wafanyabiashara wenzao kutoka katika mikoa mbalimbali kushiriki mgomokwa kile wanachokidai kuwepo kwa kodi kubwa ambazo ni kandamizi kwao
Wakizungumza na Storm FM wameonesha kuguswa na suala hilo na kuiomba serikali kuweka utaratibu mzuri ili kuondoa changamoto hiyo.
Makamu mwenyekiti wa wafanyabiashara soko la Katoro Peter Sanga amesema mazingira magumu ya kibiashara hasa katika ulipaji wa kodi ndiyo chanzo kikuu cha mgomo huo huku akiongeza kuwa wafanyabiashara wa katoro wanafuata maelekezo kutoka kwa viongozi wao wa ngazi za juu kitaifa.
Mchambuzi na wa masuala ya uchumi kutoka jijini Dar es salaam, Dkt. Lenny Kasoga amesema kinachoendelea hivi sasa ni mwamko mpya kiuchumi uliopo miongoni mwa watanzania huku akiongeza kuwa kupuuzwa na kutokufanyiwa kazi kwa malalamiko ya wafanyabiashara wa Kariakoo hapo awali ndio kumepelekea kuibuka kwa hali hii.