Wahalifu wavamia, kujeruhi mchana Mwingilo
21 June 2024, 10:26 am
Kukosekana kwa kituo kidogo cha polisi katika kata ya Ikunguigazi wilayani Mbogwe mkoani Geita kumetajwa kuwa ni chanzo cha vitendo vya uhalifu katika vijiji vya kata hiyo.
Na: Nicolaus Lyankando – Geita
Samwely Nestory ni mhanga wa tukio la hivi karibuni mwezi Mei, mwaka huu anasema watu wallifika nyumbani kwake na kisha kuanza kumshambulia na kumjeruhi vibaya sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kuutupa mwili wake vichakani.
Wananchi katika kijiji cha Mwingilo kata ya Ikunguigazi wilayani Mbogwe mkoani Geita wamesema wanaishi kwa hofu kufuatia matukio ya watu wasiojulikana kuvamia vyakati za mchana na kujruhi huku wakiiba baadhi ya mali zao.
Akitolea taarifa juu ya hali ya ulinzi na usalama katika kijiji hicho Mwenyekiti wa kijiji Charles Magigima amekiri matukio hayo ya mchana huku akiwataka wananchi kujilinda wao wenyewe.
Diwani wa kata ya Ikunguigazi Paulo Lutandula ameeleza hatua zilizochukuliwa hadi sasa pamoja na kuelezea changamoto ya kutokuwa na kituo cha polisi katika kata yake.