Umeme vijijini ulivyobadilisha maisha Geita
18 June 2024, 8:27 am
Na Adelina Ukugani:
Karibu katika makala ya Tafakari Pevu, kipindi kinachokukutanisha wewe msikilizaji na kiongozi wako kujadili masuala mbalimbali yanayotatiza utekelezaji wa dhana ya utawala bora Mkoani Geita.
Tafakari Pevu inatoa nafasi kwako kuibua changamoto katika eneo lako zinazokwamisha mikakati ya wananchi na viongozi kujiletea maendeleo. Tafakari Pevu inatafiti changamoto za maendeleo ya jamii kupitia visa halisi na kuvifikisha visa hivyo kwa viongozi ili vipatiwe ufumbuzi.
Kupitia kipindi hiki viongozi wa ngazi mbalimbali mkoani Geita hupata nafasi ya kutoa ufafanuzi juu ya hoja za msingi zinazoibuliwa na jamii kwa mantiki ya kujenga muafaka wa jamii juu ya uelewa wa changamoto husika, mikakati anuai na hatua madhubuti za kutatua changamoto hizo.
Makala yetu kwa siku ya leo inaangazia namna Serikali ilivyotumia fedha nyingi kufikisha nishati ya umeme vijijini hali ambayo imechangia kuleta mabadiliko nakukua kwa uchumi wa wananchi kwa kasi katika kijiji cha Ihako wilayani Bukombe Mkoani Geita.