NELICO yatoa vitimwendo 50 kwa watoto wenye ulemavu Geita
18 June 2024, 7:41 pm
Katika kupunguza changamoto kwa watoto wenye ulemavu mashirika mbalimbali mkoani Geita yameombwa kuendelea kujitokeza kulisaidia kundi hilo.
Na Mrisho Sadick – Geita
Shirika la NELICO Mkoani Geita limeadhimisha siku ya mtoto wa afrika kwa kutoa viti mwendo 50 na bima za afya 50 kwa watoto wenye ulemavu ili kuwaondolea changamoto ya kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo mkoani Geita Paulina Alex akiwa katika maadhimisho hayo leo Juni 18,2024 ambayo kimkoa yamefanyika katika kata ya Nyamigota wilayani Geita Mkoani Geita amesema viti hivyo vimegharimu fedha zaidi ya milioni 15.
Sambamba na hayo Majogoro amesema katika kuadhimisha siku ya mtoto wa afrika shirika hilo litatumia milioni 25 kusasaidia kurudisha tabasamu kwa watoto 50 waliozaliwa na tatizo la mdomo sungura nakwamba kila mtoto atagharimu shilingi laki tano (500,000).
Akizungumza kwaniaba ya mkuu wa mkoa wa Geita mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba amelipongeza shirika la NELICO kwa kuendelea kuisaidia serikali kupunguza changamoto kwa watoto wenye ulemavu nakuyataka mashirika mengine mkoani Geita kuiga mfano huo kwa maslahi mapana ya taifa.