Storm FM

DC Geita atoa neno kwa wasimamizi wa miradi ya wilaya

13 June 2024, 11:14 am

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba (kati) akikagua ujenzi unaoendelea katika hospitali ya mji wa Geita. Picha na Kale Chongela.

Mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba ameendelea kufanya ziara kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya wilaya ya Geita na kukagua miradi ya maendeleo ambayo inaendelea kutekelezwa katika wilaya hiyo.

Na: Kale Chongela – Geita

Serikali wilaya ya Geita imewataka wasimamizi wa miradi kuhakikisha inakamilika kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na uwepo wa miradi hiyo.

Jengo moja wapo linalojengwa katika hospitali ya mji wa Geita. Picha na Kale Chongela

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Geita Hashim Komba juni 11, 2024 akiwa katika ukaguzi  wa ujenzi wa mradi  wa jengo la upasuaji, jengo la kuchomea taka na jengo la kuhifadhia maiti linalojegwa katika hospital ya mji wa Geita.

Sauti ya DC Geita
Jengo la kuchomea taka linaloendelea kujengwa hospitali ya mji wa Geita. Picha na Kale Chongela

Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Geita Dkt. Sunday Mwakyusa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi wa miradi hiyo itasadia kupunguza changamoto zilizopo kwa sasa.

Sauti ya Dkt. Sunday Mwakyusa

Kwa upande wake msimamizi wa miradi hiyo kutoka halmashauri ya mji wa Geita mhandisi Hamza Said amesema miradi hiyo inatarajia kukamilika mwezi septemba mwaka huu.

Sauti ya msimamizi mradi