Storm FM

Wananchi mjini Geita wakerwa na tabia za bodaboda

13 June 2024, 10:25 am

Baadhi ya waendesha pikipiki mkoani Geita. Picha na maktaba ya Storm fm

Usafiri wa pikipiki maarufu bodaboda umeendelea kurahisisha maisha ya wananchi wengi kutokana na uharaka wa kufika kutoka eneo moja hadi linguine huku ukitoa ajira kwa baadhi ya vijana.

Na: Amon Mwakalobo – Geita

Baadhi ya wananchi katika halmashauri ya mji wa Geita wamelalamikia tabia ya baadhi ya waendesha pikipiki kwa tabia ya kuburuza makopo yaliyotumika barabarani huku wakiwa wanaendesha pikipiki zao kwa mguu mmoja hali inayopelekea kelele na taharuki kwa wananchi

Storm FM imezungumza na wananchi hao Juni 12, 2024 ambapo wamesema wamejaribu kuwaonya na kuwashitaki kwa baadhi ya wenyeviti wa maegesho yao ya kazi lakini hali bado inaendelea.

Sauti ya wananchi

Baadhi ya madereva wa pikipiki akizungumza kwa niaba ya wenzake Joseph Mussa amesema kuwa wanafanya kwa utani tu huku wengine wakieleza wanapata motisha ya kazi wanapofanya hivyo.

Sauti ya bodaboda

Mwenyekiti wa waendesha pikipiki kata ya Kalangalala Hanschadius Valentine amesema malalamiko hayo wameyapata watafanyia kazi suala hilo.

Sauti ya mwenyekiti