Barabara ya Ushirombo-Nyikonga hadi Katoro kuanza kujengwa
10 June 2024, 3:51 pm
Serikali imedhamiria katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara ambazo zimeharibika kutokana na mvua zilizonyesha nchini ili kuweka urahisi kwa wananchi kutumia barabara hizo.
Na: Edga Rwenduru – Geita
Serikali imeanza mpango wa kujenga barabara ya Ushirombo-Nyikonga mpaka Katoro kwa kiwango cha lami zikiwa ni jitihada za serikali kuboresha miundombinu ya barabara ambayo kwa kiasi kikubwa imeharibiwa na mvua.
Akiitimisha ziara ya siku tatu Juni 8, 2024 katika jimbo lake la Bukombe Naibu waziri mkuu na mbunge wa jimbo la Bukombe Doto Biteko akiwa ameambatana na waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa katika kata ya Katome, Bashungwa alisema barabara hiyo inajengwa kwa kiwango cha lami kupitia mradi wa rise.
Aidha Bashungwa ameongeza kuwa serikali itajenga barabara ya njia nne Kutoka mwanza mjini hadi Daraja la JPM linaloendelea kujengwa Busisi ili kuondoa changamoto ya foleni ya magari.
Naibu wa Waziri mkuu Dkt. Doto Biteko amesema wizara ya ujenzi inahitaji zaidi ya Trioni Moja ili kufanyia marekebisho barabara zote zilizo haribiwa na Mvua.