Storm FM

Watoto yatima wapatiwa msaada Nyangh’wale

3 June 2024, 1:20 pm

Watoto yatima waliopatiwa msaada wa vifaa vya shule. Picha na Edga Rwenduru

Uhaba wa vifaa vya kujifunzia na mazingira duni ya kuishi bado ni kikwazo kwa watoto yatima na watoto waishio katika mazingira magumu.

Na: Egda Rwenduru – Geita

Kikundi cha Firidausi kinachoundwa na umoja wa vijana wa dini ya kiislamu wilaya ya Nyanghw’ale mkoani Geita kimetoa msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaoishi mazingira magumu pamoja na watoto yatima.

Akizungumza wakati wakikabidhi vifaa hivyo katika shule ya msingi Kharumwa wilayani humo, katibu wa kikundi hicho Hamimu Bakari amesema vifaa hivyo vimegharimu zaidi ya shilingi milioni moja na vimetolewa kwa wanafunzi 26 kwenye shule nne tofauti.

Sauti ya katibu wa kikundi
Shekhe mkuu wilaya ya Nyangh’wale Hajj Abdul akikabidhi vifaa kwa watoto. Picha na Edga Rwenduru

Aidha katika hatua nyingine Shekhe mkuu wa wilaya ya Nyanghw’ale Hajj Abdul Ramadhani Kidesela amesema Sadaka ya kweli ni kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Sauti ya Sheikh mkuu

Baadhi ya wazazi na walezi wa watoto hao wanaelezea changamoto wanazozipitia katika malezi ya watoto hao.

Sauti ya wazazi na walezi

Kwa upande wake afisa ustawi wa jamii wilaya ya Nyangh’wale Zaituni Kiboga ameviomba vikundi mbalimbali kuendelea kutoa msaada kwa watoto yatima kwani asilimia kubwa ufaulu wao upo chini kutokana na kukosa mahitaji muhimu ya shule huku wengine wakilazimika kukatisha masomo kutokana na hali ngumu ya maisha katika familia zao.

Sauti ya afisa ustawi