TAS yatoa tamko baada ya mtoto mwenye ualbino kujeruhiwa
9 May 2024, 3:36 am
Tukio la kujeruhiwa mtoto (10) mwenye Ualbino mkazi wa mtaa wa Mtakuja kata ya Katoro wilayani na mkoani Geita limekiibua Chama cha watu wenye Ualbino (TAS) wilaya ya Geita.
Na: Evance Mlyakado – Geita
Katibu wa TAS wilaya ya Geita ameeleza hatua stahiki zilizochukuliwa na chama hicho kufuatia tukio hilo pamoja na mikakati ya kuwasaidia watu wenye Ualbino ili kujilinda na watu wenye nia ovu dhidi yao.
Viongozi wa waganga wa tiba asili kwa kanda ya ziwa wametoa tamko lao kuhusu maoni mseto yanayoendelea katika jamii ambapo vitendo hivyo huhusishwa na imani za kishirikina.
Akithibitisha tukio hilo, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita SACP Safia Jongo alieleza kuwa majeraha ya mtoto na silaha iliyokutwa eneo la tukio ni wazi aliyefanya tukio hilo hakuwa na lengo la kuondoka na kiungo chochote.