Geita queens yavuna alama 1 ligi ya wanawake
30 April 2024, 6:04 pm
Ikiwa ni mwendelezo wa Ligi kuu ya wanawake Tanzania bara, Geita queens yaonesha matumaini kwa kupata sare.
Na: Juma Zacharia – Geita
Kikosi cha Geita Gold Queens kutoka mkoani Geita kimeendelea kukosa ushindi katika mwendelezo wa ligi kuu wanawake Tanzania bara.
Kikosi hicho kimeshuka dimbani April 29 kucheza na Baobab queens kutoka Dodoma na kuondoka na alama 1 baada ya sare ya goli 1-1 mchezo uliochezwa uwanja wa shule ya wasichana Nyankumbu uliopo Geita mjini.
Baada ya kukamilika kwa dakika 90 za mchezo, kocha wa Geita queens Jullius Richard amesema wamejitahidi kutafuta alama 3 lakini wanaipongeza Baobab queens ilivyocheza huku akiamini bado timu hiyo itasalia ligi kuu.
Teddy Thomas mchezaji wa Geita queens akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake amesema ulikuwa mchezo mgumu na mwalimu aliwasisitiza kushambulia zaidi
Kwa upande wa Baobab queens, kocha mkuu Paul Domician amesema wamecheza na timu nzuri sababu Geita queens ipo nafasi za chini katika msimamo hivyo inaleta ushindani.
Naye nyota na nahodha wa Baobab queens, Zuhura Khamis baada ya kuvuna alama moja amesema ulikuwa mchezo mzuri lakini hawakutumia nafasi walizozipata