Amani na upendo vyasisitizwa sikukuu ya Eid
10 April 2024, 6:21 pm
Viongozi mbalimbali wa serikali na dini wametoa Jumbe mbalimbali katika sikukuu ya Eid huku suala la kudumisha amani ya nchi likipewa uzito wa aina yake.
Na Kale Chongela – Geita
Waumini wa dini ya kiislamu mkoani Geita wametakiwa kuendelea kuishi katika matendo yaliyo mema kama ambavyo ilikuwa kwenye mwezi mutukufu wa Ramadhan.
Wito huo umetolewa na Sheikh wa Mkoa wa Geita Alhad Yusuf Kabaju kwenye Ibada ya sikukuu ya EID -AL-FITR iliyofanyika katika Uwanja wa CCM Kalanagalala Mjini Geita ambapo mgeni mwalikwa alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela ametumia fursa hiyo kwa kuwataka wananchi mkoani Geita kuendelea kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ili atimize malengo aliyo nayo kwa watanzania.
Mwandishi wetu Kale Chongela ameripoti zaidi