Mbio za baiskeli kupamba tamasha la Chato utalii festival
16 November 2023, 2:17 pm
Chato imedhamiria kukuza uchumi wake kupitia utalii kwa kutangaza vivutio vilivyopo katika eneo hilo kupitia matamasha mbalimbali ikiwemo la Chato Utalii Festival.
Kuelekea katika tamasha la Chato Utalii Festival Novemba 26 mwaka huu , Mkuu wa wilaya ya Chato Deusdedit Katwale amesema mbio za Baiskel za mashabiki wa Simba na Yanga zitatumika kuenzi nakuendeleza utamaduni wa watu wa Kanda ya Ziwa.
Katwale amesema hayo katika shindano la utangulizi la mbio za Baiskel kwa Mashabiki wa Simba na Yanga katika Kata ya Buseresere wilayani humo ikiwa ni sehemu ya maandalizi Kuelekea katika tamasha hilo Novemba 26 hadi Disemba tatu mwaka huu katika viwanja vya Magufuli mjini Chato.
Kwa upande wake Katibu wa Chama cha waendesha Baiskeli Mkoa wa Geita Raphael Ngereja amesema katika shindano hilo la utangulizi wamepata washindi 10 kati ya 20 waliyoshiriki ambao watauwakilisha mkoa wa Geita katika mashindao ya Chato Utalii Festival ambapo kunatakuwa na washiriki wengine kutoka Mwanza na Simiyu.
Mbio hizo za Kilometa 34 zimeanzia Kata ya Buseresere hadi Kata ya Bwanga zilikuwa na washiriki 20 huku mshindi wa kwanza akiwa ni Onana Amos Shabiki wa Simba amesema ataendelea kufanya mazoezi zaidi ili kujiandaa na mashindano rasmi.