Wanafunzi kidato cha nne wapewe nafasi na uhuru wakati wote wa mtihani
13 November 2023, 11:41 am
Kuanza kwa mtihani wa kidato cha nne kumeisukuma taasisi ya mtetezi wa mama wilayani Geita kuandaa kongamano la kuwaombea nakuwapatia vifaa watahiniwa katika shule za Katoro na Ludete.
Na Mrisho Sadick:
Wazazi na walezi Mkoani Geita wametakiwa kuwatimizia mahitaji ya msingi nakuwapunguzia majukumu wanafunzi wa kidato cha nne wanaotarajia kuanza mtihani wa Taifa Novemba 13 mwaka huu ili kuwapa nafasi ya kujiandaa vizuri.
Rai hiyo imetolewa na viongozi wa dini na wakuu wa Shule za Sekondari Katoro na Ludete wilayani Geita katika kongamano la kuwaombea nakuwapatia vifaa mbalimbali wanafunzi wa kidato cha nne lililoandaliwa na taasisi ya Mtetezi wa mama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu Mkoani Geita.
Mwenyekiti wa taasisi ya mtetezi wa mama wilaya ya Geita Elizabeth Coster amesema sambamba na Kongamano hilo Taasisi hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo huku kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Safia Jongo akisema vitendo vya uaktili ikiwemo ubakaji vimeendelea kupungua.