Kilometa 17 za lami kumaliza changamoto ya miundombinu ya barabara mjini Geita
26 October 2023, 4:18 pm
Baada ya wananchi wa baadhi ya maeneo ya Halmashauri ya Mji wa Geita kulia na changamoto ya miundombinu ya barabara sasa serikali imesikia kilio chao.
Na Kale Chongela:
Halmashauri ya mji wa Geita kupitia mradi wa uboreshaji miji TACTIC imeanza ujenzi wa barabara kilometa 17 kwa kiwango cha lami ili kuondoa changamoto ya usafirishaji watu na bidhaa ndani ya mji wa Geita.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala wa barabara za mjini na vijini TARURA wilaya ya Geita Mhandisi Bahati Subeya katika mkutano uliowakutanisha viongozi mbalimbali wa kata nne ambazo zitanufaika na mradi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita Costantine Morandi ametumia fursa hiyo kuwataka wakandarasi kuanza kutelekeza barabara hizo kwa wakati kwani yapo baadhi ya maeneo korafi hivyo inatakiwa kazi ifanyika kwa kasi
Mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Cornel Magembe ametoa msistizo kwa TARURA Kujenga desturi ya kukagua barabara hizo kila wakati ili zijengwe kwa kiwanga kinachotakiwa.
Barabara hizo ni Mkolani – Mwatulole Kilometa 5.9 , Nyankumbu – Kivukoni Kilometa 3.9 , Nguzombili -Samandito – Emma – Mama Kengele kilometa 3.3 na Mwatulole – Nshinde – Twiga – GGR 3.9.