Storm FM

Vijiji 75 wilaya ya Geita vyapatiwa umeme

3 October 2023, 11:04 am

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Madini Dkt Biteko akiwasha umeme katika vijiji vya Nyanguku na Bunegezi wilayani Geita. Picha na Mrisho Sadick

Dhamira ya serikali ya awamu ya sita nikufikisha umeme katika vijiji zaidi ya elfu 12 hapa nchini imeendelea kuonekana baada ya serikali kuendelea kufikisha huduma hiyo vijijini.

Na Mrisho Sadick:


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imefikisha nishati ya umeme kwenye vijiji 75 kati ya 145 vya wilaya ya Geita ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya serikali kufikisha umeme katika vijiji vyote vya Tanzania.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa nishati Dkt. Dotto Biteko ameendelea na ziara yake ya kuwasha umeme vijijini, akiwa katika vijiji vya Nyanguku na Bunegezi wilayani Geita amesema serikali ya awamu ya sita imekusudia kuwainua Wananchi kiuchumi kwa kuwasogezea huduma muhimu kama umeme, maji na miundombinu ya barabara vijijini ili kuchochea uzalishaji mali.

Sauti ya Naibu Waziri Mkuu

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amesema uwepo wa umeme katika kijiji cha Nyanguku na Bunegezi kutasaidia kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji huku Mkurugenzi wa umeme vijijini Jones Olotu akisema kasi ya usambazaji umeme katika vijiji vya jimbo la Geita mjini inaendelea.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Geita

Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Constantine Kanyasu ameishukuru serikali kwa hatua hiyo huku Diwani wa kata ya Nyanguku Elias Ngole akimuomba Naibu Waziri Mkuu kuongeza nguvu ya usambazaji wa umeme katika vijiji ambayo bado havijafikiwa na nishati hiyo.