Mgodi wa GGML umetoa madawati 3,000 shule za msingi wilayani Geita
26 July 2023, 7:39 pm
Kutokana na changamoto ya upungufu wa madawati katika shule za msingi wilayani Geita Mgodi wa GGML umejitosa kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto hiyo.
Na Kale Chongela:
Mgodi wa Geita Gold Mining Limited GGML umekabidhi madawati 3,000 kwa ajili ya shule za msingi katika Halmashauri za wilaya ya Geita na Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita ili kukabiliana na changamoto ya upungufu katika shule hizo.
Zoezi la kukabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela limeongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa GGMlL Terry Strong katika viwanja vya ofisi za uwekezaji EPZA mjini Geita na limehudhuriwa na viongozi mbalimbali pampja na wanafunzi.
Awali kabla ya kukabidhi madawati hayo Mkurugenzi Mtendaji wa GGMlL Terry Strong amesema Mgodi huo umeahidi kukabiliana na changamoto ya upungufu wa madawati katika shule ya msingi nakwamba watatoa madawati 8,000 na wameanza kwa kukabidhi madawati 3,000.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela ameupongeza mgodi huo kwa kuendelea kushirikiana na serikali ya mkoa wa Geita katika utatuzi wa changamoto mbalimbali katika jamii nakwamba madawati hayo yatakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa wilaya ya Geita nakumuagiza afisa elimu wa mkoa wa Geita kuwa yakatunzwe ili yatumike kwa muda mrefu.