Mwitikio kuchangia damu Geita mjini ni mdogo
24 July 2023, 1:19 pm
Uhitaji wa damu salama katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita ni Mkubwa kuliko inayopatikana kutoka kwa watu wanaochangia.
Na Kale Chongela:
Mwitikio wa wananchi kuchangia damu salama bado ni Mdogo ukilinganisha na uhitaji katika Hospitali ya halmashuri ya mji wa Geita.
Kauli hiyo imetolewa na Msimamizi wa kitengo cha damu salama katika Hosptali hiyo Shabani Makoye katika zoezi la uchangiaji wa damu lililofanywa na mashabiki wa Yanga katika Mtaa wa Mgogo B kata ya Buhalahala Mjini Geita.
Baadhi ya wananchi waliyoshiriki katika zoezi hilo la uchangiaji wa damu wametumia fursa hiyo kuwataka wananchi na jamii kuendelea kwakuwa uhitaji ni mkubwa.
Mwenyekiti wa tawi la Yanga Mtaa wa Magogo “B” Robert Sungura amesema amewahamasisha wananchama wake juu ya umuhimu wa kuchangia damu ili kuokoa vifo vya watu wenye uhitaji wa damu.