Auziwa mtungi wenye unga wa muhogo kwa ndani
16 July 2023, 1:17 pm
Matukio ya utapeli katika nyanja mbalimbali yamekithiri ikiwamo katika upande wa upatikanaji wa vifaa vya kuzimia moto na uokoaji, jambo lililomuinua Inspekta Lukuba kuzungumzia hilo.
Na Kale Chongela- Geita
Jeshi la zimamoto na ukoaji mkoni Geita limewataka wananchi kufika katika ofisi za zimamoto pindi wanapohitaji kununua vifaa vya kuzimia moto ili kuepukana na vishoka.
Wito huo umetolewa na Kaimu kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoani Geita Inspekta Edward Lukuba akiwa ofisini kwake ambapo amesema pamekuwepo na matepeli ambao wamekuwa wakiwauzia wananchi vifaa vya kuzimia moto vyenye unga wa mhogo kwa ndani.
Aidha Inspekta Lukuba amesema wapo mawakala ambao wamependekezwa na Jeshi hilo kwa ajili ya kuuza vifaa vya kuzima moto huku akiwataahadharisha wananchi kuepuka matepeli.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi mjini Geita wamesema endapo elimu itazidi kutolewa mara kwa mara itasaidia kwa haraka kufahamu namna ya kutambua kifaa bora cha kuzima moto, sambamba na namna ya kutumia kifaa hicho pindi moto unapotokea.