Wananchi wacharuka kuuziwa nguzo za umeme
15 July 2023, 6:51 pm
Ukubwa wa gharama za umeme katika maeneo mbalimbali ya vijijini ni moja ya changamoto inayowanyima fursa wananchi kupata huduma ya umeme.
Na Nicolaus Lyankando- Geita
Wananchi wanaoishi maeneo ya vijijini katika halimashauri ya wilaya ya mbogwe mkoani Geita wamelalamikia gharama kubwa wanazotozwa kufikishiwa huduma ya Umeme nakudai kuna mianya ya rusha hufanyika katika zoezi hilo.
Wakizungumzia changamoto hiyo baadhi ya wananchi wilayani mbogwe wamesema gharama za kufikiwa na huduma hiyo kwa sasa ni kubwa nawao imekuwa vigumu kuimudu gharama hiyo huku wakisema wamekuwa wakitozwa mpaka gharama za kulipia nguzo jambo ambalo limewatia mashaka huenda kunauonevu kwa wananchi wenye hali ya chini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Nyikonga moja ya vijiji vilivyofikiwa na huduma hiyo
Mperwa Sekela amekiri kukumbana na kesi za mara kwa mara kwa wananchi juu ya gharama
hizo nakuiomba serikali isikie kilio cha wananchi hao.
Akitolea majibu ya malalamiko Hayo meneja wa shirika la Umeme TANESCO wilani humo
Fabian Lukiko kwanza ameanza kwa kukanusha nakusema hakuna gharama anayotoa
mwananchi kwajili ya nguzo ya umeme.
Halimashauri ya wilaya ya Mbogwe ina zaidi ya vijiji 83 na zaidi ya nusu ya vijiji hivyo
imeshafikiwa na huduma ya umeme.