Ahadi zilizoahidiwa kwenye uchaguzi zitekelezwe
14 July 2023, 4:24 pm
Katika uchaguzi wa wa uongozi katika nyadhifa mbalimbali ukiwemo wa mtaa, viongozi hunadi sera zao kwa wananchi ili waweze kupigiwa kura za kuwahudumia wananchi wa eneo husika, Je ahadi huwa zinatekelezwa?
Na Zubeda Handrish- Geita
Kufuatia utaratibu wa Kipindi cha Storm Asubuhi kilichopo Storm FM chenye utaratibu wa kila Ijumaa kuzungumza na wananchi wa serikali za mitaa na vijiji juu ya mambo waliyoahidiwa wakati wa uchaguzi na ni kwa namna gani yametekelezwa na kiongozi wa mtaa au kijiji husika ambaye ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa au kijiji ambapo mpango huo tumeupa jina la “Agenda 2019” , leo tumeanza na mtaa wa Shilabela uliopo kata ya Buhalahala, halmashauri ya mji wa Geita.
Wananchi wa mtaa huo wa Shilabela wamezungumza kwa kina juu ya ahadi zilizotekelezwa na zisizotekelezwa.
Baada ya wananchi kuzungumzia ahadi hizo na utekelezaji wake, Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Shilabela Bw. Fredrick Andrea Masalu nae amejibia hoja za wananchi wa mtaa wake, huku moja ya jambo alilotekeleza licha ya kwamba bado halijakamilika ni ukarabari wa barabara za mitaa mtaani hapo pamoja na ukarabati wa soko.
Mwenyekiti Masalu pia amezungumzia suala zima la usafi wa mazingira alivyouimarisha mtaani hapo pamoja na utoaji wa taarifa juu ya mapato na matumizi a mtaa wake.
Pia amejibia suala la Zahanati na Soko, na namna alivyopambania ajira kwa vijana wa mtaa wake.