Waendesha bodaboda watoa ya moyoni.
9 August 2021, 3:47 am
Na Zubeda Handrish:
Waendesha pikipiki maarufu Bodaboda mjini Geita wamewalalamikia vitendo vya baadhi ya abiria wenye tabia ya kusema uongo pindi wanapohitaji huduma hiyo ya usafiri.
Wameyasema hayo katika egesho lao la kazi la Shilabela Msikitini kuwa baadhi ya abiria husema uongo sehemu anayoelekea kwa kuhofia kutoa pesa kubwa na hivyo kuwarudisha nyuma kimaendeleo.
Katibu wa bodaboda katika egesho hilo amewaasa bodaboda hao kukubaliana kwanza na abiria kabla ya kuanza safari ili kuepukana na vuruguzisizokuwa za lazima na kujilindia heshima katika kazi yao.
Aidha abiria wanaotumia vyombo hivyo vya usafiri wamekiri kuwepo kwa changamoto hiyo lakini sababu kubwa baadhi ya abiria wanakuwa wageni sehemu wanazoelekea.