Tunakabiliwa na changamoto nyingi:
8 July 2021, 8:43 pm
Wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika Kata ya Nyarugusu wilayani Geita wameiomba serikali kuendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili ikiwemo nishati ya umeme pamoja na kusogeza huduma ya ofisi ya madini katika eneo hilo.
Wakizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita baadhi ya wachimbaji hao katika mgodi wa Nsangano Mining uliyopo kata ya Nyarugusu wameiomba serikali kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili ili kurahisisha utendaji wa kazi zao.
Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Nsangano Bw Nsangano amesema uwepo wa Mgodi huo katika eneo hilo umekuwa chachu ya ajira kwa wakazi wa kata hiyo pamoja na mapato serikali.
Kwa upande wake Afisa Madini wa Mkoa wa Geita Bw Daniel Mapunda amesema Ofisi yake imeendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabili wachimbaji hao.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Bi Rosemery Senyamule amesema serikali ipo kwa ajili ya kutatua kero za wananchi mbalimbali zinazowakabili nakuwahakikishia kuwa atawapa ushirikiano.