TWCC Yawatembelea Wanawake Migodini
7 June 2021, 6:57 pm
Na Zubeda Handrish:
Katika kuendelea kuwainua wafanyabiashara wadogo wanawake kwa upande wa Uchimbaji,Mkurugenzi Mtendaji Wa Chama Cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) Bi Mwajuma Hamza ametembelea machimbo madogo ya Dhahabu ya Mgusu, Msasa na Nyarugusu Mkoani Geita
Akizungumza na Strom FM amesema dhamira kubwa ya ziara hiyo katika machimbo hayo ni kutambua changamoto wanazopitia wanawake hasa machimboni na namna ya kuweza kutatua ili kumuwezesha mwanamke kunufaika na shughuli za uchimbaji
Mwenyekiti wa wachimbaji wanawake kwa upande wa Mgusu Bi Bernadeta Furgence Petro amezungumzia changamoto na hali ilivyo ya uchimbaji kwa wanawake migodini na kusema moja ya changamoto ni kukosa vitendea kazi
Bi Jovina Jovinary anayefanya shughuli zake mgodini ametoa shukrani kwa ujio wa viongozi hao na kutoa wito kwa wanawake wenzie kuchangamkia fursa hususani za mafunzo ili kuongeza ufanisi, ubora na kupata uewelewa juu ya shughuli wanazofanya.
Katika hatua nyingine wachimbaji kutoka katika migodi ya Mgusu, Msasa na Nyarugusu wamezungumzia changamoto na kazi zao zinavyokwenda na kuiomba Taasisi hiyo kuwasaidia kuwapatia zana kwaajili ya kazi.