Wanaume watakiwa kujitokeza kufanyiwa tohara Geita
28 May 2021, 2:10 pm
Wanaume ambao hawajafanyiwa tohara Mkoani Geita wameshauriwa kujitokeza katika vituo vya afya kupatiwa huduma hiyo kwani inasaidia kujikinga na magonjwa mbalimbali ikiwemo kupunguza 60% ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa kuthibiti Ukimwi Mkoani Geita Dkt Furaha Kibaba wakati akizungumza na Storm FM Ofisini kwake ambapo amesema mwitikio wa wanaume kujitokeza kupata huduma hiyo mkoani Geita ni mzuri na kuwashauri ambao bado wafike katika maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo kwani huduma hiyo inatolewa bure.
Katika Hatua Nyingine Dkt Kibaba ameongeza kwa kusema kuwa kwa mujibu wa Takwimu za wanaume kufanyiwa tohara mkoani Geita mwaka 2020 kwa kuanzia mwezi januari hadi disemba zinaonesha kuwa wanaume Elfu 47,488 katika mkoa mzima wa Geita walifanyiwa tohara.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi Mkoa wa Geita wamesema licha ya huduma hii kutolewa bure bado shughuli za utafutaji mali zinawafanya kushindwa kutimiza adhima hiyo.