Wachimbaji Watakiwa Kuondoa Migogoro Kazini
21 May 2021, 5:52 pm
Na Joel Maduka:
Wachimbaji wadogo ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao kwenye Mikoa ya Kanda ya ziwa wametakiwa kuondoa tofauti ambazo zimekuwa zikisababisha migogoro ya mara kwa mara hali inayochangia kushindwa kuungana ili kuweza kukuza uzalishaji wao na kuufanya kuwa wenye tija kutokana na mchango mkubwa ambao wamekuwa wakiutoa kwenye sekta ya uchumi wa taifa.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha wakati akifungua Mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka Mikoa ya Geita, Mwanza na Shinyanga ambayo yameandaliwa na taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo FADEV ambapo lengo lake ni kusaidia kuandika habari ambazo zitawasaidia wachimbaji wadogo kufata kanuni na sheria za uchimbaji salama.