Wazazi na Walezi Wagomea Chanjo Nyankumbu, Geita
20 May 2021, 8:05 pm
Na Mrisho Sadick:
Wazazi na walezi katika mtaa wa uwanja kata ya Nyankumbu mjini Geita wameshauriwa kuwaruhusu watoto wao kupatiwa dawa za kinga tiba ya kichocho na minyoo ili kuwakinga na changamoto hiyo.
Rai hiyo imetolewa na Mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha nyankumbu Dkt Amon Malanga kufuatia baadhi ya wazazi katika mtaa wa uwanja kukataa watoto wao kupatiwa dawa hizo kwa kile walichokieleza kuwa hawana imani nazo.
Wakiwa katika mkutano wa mtaa katika shule ya msingi ukombozi baadhi ya wazazi waliokata dawa hizo wamesema hawana imani kuwa zinaweza kuwasaidia watoto wao.
Baadhi ya wazazi waliyokubali watoto wao kupewa dawa hizo wamewashauri wazazi wenzao kukubali mpango huo ili kuwakinga watoto wao na matatizo ya minyoo na kichocho.
Diwani wa kata ya Nyankumbu Bw John Mapema amesema anaheshimu mawazo ya wananchi wake kuhusu uamuzi wao wa kukataa ama kukubali dawa hizo nakutumia nafasi hiyo kuwaasa wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wao kupatiwa dawa hizo.