Kikundi cha WhasApp cha Geita Huru chatoa msaada
13 May 2021, 9:47 am
Na Mrisho Sadick:
Kikundi cha WhatsApp cha Geita Huru kimeungana kwa pamoja kuwatembelea watoto wenye uhitaji wakiwemo yatima katika kituo cha Bright Light kilichopo Geita mjini ambapo wametoa msaada wa chakula na vifaa vya usafi kwa ajili ya watoto hao.
Wakizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo wawakilishi wa kikundi hicho wamesema wamelazimika kutumia kikundi hicho kwa manufaa ya jamii ikiwemo kusaidia watu wenye uhitaji nakwamba wataendelea kushirikiana kwa pamoja kusaidia makundi mbalimbali yenye uhitaji wakiwemo wafungwa.
Akizungumza kwa niaba ya watoto Mkurugenzi wa Kituo hicho Methew Daniel amewapongeza wanakikundi wa Geita Huru kwa kuungana kwa pamoja nakutoa msaada wa watoto hao nakutumia fursa hiyo kuwaomba watu wengine kuendelea kujitokeza kuwasaidia watoto hao.