Mgogoro wa mipaka kikwazo cha Maendeleo
27 April 2021, 1:53 pm
Na Nichoras Paul Lyankando:
Matumaini ya kumalizika kwa mgogoro wa mipaka ya kijiji cha lulembela na nyikonga wilayani mbogwe mkoani geita yameanza kuonekana mara baada ya viongozi wa kata husika kuingilia kati.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliowakutanisha wananchi katika kijiji cha nyikonga kata ya lulembela uliyo andaliwa na diwani wa kata hiyo Bw Deus Lyankando wamesema mgogoro huo umedumu kwa mda mrefu mpaka sasa kutokana na kaya zilizopo mpakani mwa vijiji hivyo kukwepa michango kwa kisingizio cha kuwa upande mwingine na wakaomba kueleweshwa mwisho wa mipaka ya vijiji hivyo.
Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa kijiji cha nyikonga Bw MPERWA SEKELA Amesema imewapa wakati mgumu wao kama viongozi kutambua idadi halisi ya kaya pindi wanapoanzisha miradi ya kimaendeleo ya kuchangiwa na wananchi na hivyo wameomba kubainishiwa mipaka halisi ya vijiji hivyo ili waanze uhakiki upya wa kaya.