Wanasoka Geita waomba kujengewa uwanja wa kisasa
21 April 2021, 11:15 am
Na William Petro:
Mashabiki na wapenzi wa wa soka mkoni Geita wameuomba uongozi wa mkoa kuangalia namna ya kukamilisha ujezi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu kwani miundombinu ni sehemu ya maendeleo ya soka.
Wapenzi na mashabiki hao wamesema sio ishara nzuri kwa mkoa wenye timu inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara kukosa uwanja kwani Geita ni miongoni mwa mikoa michache nchini isiyokuwa na viwanja vya kisasa vya soka.
Katika hatua nyingine mashabiki hao wameendelea kuwa na imani na timu ya Geita Gold FC inasyoshiriki ligi daraja la kwanza nchini baada ya kuwa vinara wa kundi B na kuwataka viongozi kuhakikisha wanaisaidia timu hiyo kupanda ligi kuu msimu huu.
Geita Gold FC itashuka dimbani jumapili ya 25/04/2021 dhidi ya Transt Camp ya jijini Dar es salaam kabla ya kuvaana na Kitayoske FC , Rhino Rangers na Fountain Gate FC ili kukamilisha duru ligi daraja la kwanza tanzanai bara 2020/21.