Shule mpya ya sekondari kuondoa changamoto Geita
16 April 2021, 6:23 pm
Na Mrisho Sadick:
Kukamilika kwa ujenzi wa shule ya sekondari Evarist iliyopo kata ya nyarugusu wilayani Geita umesaidia kupunguza mrundikano wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya nyarugusu iliyopo katani humo.
Akizungumza na Storm FM shuleni hapo afisa elimu wa kata ya Nyarugusu Bw Robert Loti amesema shule hiyo imejengwa na serikali kwa kushirikiana na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu wa mgodi wa Stamico, nakupewa jina la Evaristi ambae ni mkurugenzi wa mgodi huo kwa kufanikisha ujenzi huo kwa asilimia kubwa.
Mkuu wa shule hiyo Bw Fred Benedict amesema wanafunzi waliochaguliwa kujiunga katika shule hiyo ni 300 ikiwa wavulana 173, wasichana 127 huku walioripoti wavulana ni 152 sawa na asilimia 85 wasichana 104 sawa na asilimia 15 .
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyarugusu Bw Vitus Issack amesema kukamilika kwa shule hiyo kumesaidia kupunguza changamoto katika katika shule ya sekondari ya nyarugusu na amewapongeza wadau waliosaidia ujenzi wa shule hiyo.