Geita Gold FC yaapa kupanda ligi kuu 2021/22
16 April 2021, 6:06 pm
Na William Petro:
Klabu ya soka ya Geita Gold FC ya mkoani Geita inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara imesema kuwa mchezo wake wa kesho 17/04/2021 dhidi ya Pamba FC ya Mwanza ndio otakatoa hatima ya klabu hiyo kupanda kwenda ligi kuu ya soka Tanzania bara 2021/22.
Kocha mkuu wa Geita Gold FC Fred Felix Minziro amesema rekodi ya kutokupoteza mchezo wowote kwenye uwanja wa nyumbani wa Nyankumbu inawapa faraja ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo dhidi ya Pamba utakaopigwa kuanzia majira ya saa 10 alasiri na kuwataka wanageita kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao.
Nao mashabiki wa timu hiyo wameonyesha kufurahishwa na mwenendo wa timu yao msimu huu hasa inapocheza kwenye kwenye uwanja wa nyumbani n awa imani kuwa timu hiyo itibuka naushindi na kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kupanda ligi kuu msimu wa 2021/22.
Gieta Gold FC wako nafasi ya pili katika msimamo wa kundi B ligi daraja la kwanza wakiwa na alama 25 nyuma ya vinara Pamba FC wenye alama 27 na wanahitaji kushinda mchezo wa kesho ili kuwashusha Pamba waliokaaa kwenye kilele kwa zaidi ya miezi mitatu.