Takukuru Mkoani Geita yaokoa zaidi ya Million 300
16 April 2021, 5:56 pm
Na Joel Maduka:
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Geita kwa Kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi 2021 imefanikiwa kuokoa kiasi cha zaidi ya Tanzania shilingi milioni miatatu ambazo zilikuwa zimefanyiwa ubadhirifu kwa njia mbalimbali za rushwa ,dhuluma na nyinginezo.
Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye viunga vya ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Geita, Mkuu wa Takukuru Mkoani humo LEONIDAS FELIX amewataka watumishi wa umma pamoja na waajiri kufuata taratibu za kupeleka fedha za mifuko ya jamii kwa wakati.
Nao baadhi ya waliokuwa wafanyakazi kwenye kampuni ya Kyang’ani wameishukuru Taasisi hiyo kwa Jitihada ambazo wamezifanya na kufanikisha kupatiwa stahiki za fedha ambazo walikuwa wakizidai.