Watoa huduma ya chakula mitaani watakiwa kuvaa sare Geita
15 April 2021, 5:50 pm
Na Kale Chongela:
Watoa huduma ya chakula katika halmashauri ya mji wa Geita wametakiwa kuvaa mavazi maalum wakati wa biashara pamoja na kofia kwa ajili ya kuimarisha usafi ili kuendelea kulinda afya za wateja wanaowahudumia.
Wito huo umetolewa na Afisa Afya wa kata ya Mtakuja Bw Edward Mwita ambapo amebainisha kuwa ni vyema kuendelea kuzingatia suala la mavazi kwa watoa huduma ya chakula ili kuimarisha usafi sambamba na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Wakielezea baadhi ya watoa huduma kwenye migahawa wamesema licha ya uwepo wa changamoto ya kiuchumi wameahidi kuzingatia taratibu na kanuni ambazo zinatolewa na idara ya afya ili kuweza kuepukana na mvutano.
Aidha baadhi ya wananchi mjini Geita wamesema endapo suala la usafi wa mazingira likizingatiwa katika huduma za utoaji wa chakula itasaidia kuondokana changamoto ya magonjwa ya mlipuko.