Matundu 12 ya Vyoo kuondoa changamoto
14 April 2021, 7:16 pm
Na Paul Lyankando:
Wananchi katika kijiji cha ikunguigazi wilayani mbogwe mkoani geita wamekamilisha ujenzi wa matundu 12 ya vyoo vya kisasa katika shule ya msingi ikunguigazi ili kunusuru zaidi ya wanafunzi 899 kujisaidia hovyo.
Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa ujenzi huo katibu wa kamati ya ujenzi katika kijiji hicho Bi Rosemary James amesema wamekamilisha ujenzi wa matundu 12 ya vyoo vya kisasa ambayo yamegharimu zaidi ya shilingi milioni 6 ambazo zimechangwa na wananchi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Jumanne Manyasa amesema katika ujenzi huo kumekuwepo na mwitikio mkubwa wa wananchi kujitolea hali ambayo ili chochea kukamilika mapema kwa vyoo hivyo ambapo mahitaji ya matundu ya vyoo katika shule hiyo ni matundu 41 huku yaliyopo kwa sasa ni matundu 24 upungufu ukiwa ni 17.
Mbali na kukamilika kwa matundu hayo ya vyoo wananchi katika kijiiji hicho wamekuwa na kilio kingine cha maji kutokana na vyoo hivyo kuhitaji maji ya kutiosha wameiomba serikali kuwachimbia visima virefu vya maji ili kuwezesha upatikanaji wa maji nakuondoa adha ya wanafunzi kutumia mda mwingi kufata maji yakutumia katika vyoo hivyo.